Kuhusu sisi
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa (ORPP) ni afisi ya serikali iliyoanzishwa chini ya Kifungu cha 260 cha Katiba ya Kenya, 2010, na Sheria ya Vyama vya Kisiasa, 2011. Majukumu ya ofisi hiyo, miongoni mwa mengine ni kudhibiti uundaji, usajili, na ufadhili wa vyama vya siasa kwa mujibu wa Katiba na utawala wa sheria.
Sheria hiyo ndiyo marejeo ya kimsingi ya kisheria ya usimamizi wa vyama vya kisiasa kwa mujibu wa Vifungu 91 na 92 vya Katiba, ambavyo vinatazamia vyama vya siasa vinavyotawaliwa vyema vinavyoheshimu demokrasia ya ndani na hadhi yao ya kikatiba katika mfumo wa kisiasa wa Kenya.
ORPP ina muundo wa shirika unaoongozwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, chini ya Wasajili Wasaidizi watatu (3). Kurugenzi zipo nne (4) ambazo ni; Usajili na Udhibiti; Usimamizi wa Fedha; Mipango, Utafiti na TEHAMA; na Usimamizi na Utawala wa Rasilimali Watu.
Historia Yetu
Vivutio muhimu vya nyakati na zamu za historia yetu vimejumuishwa kati ya mambo mengine chini ya yafuatayo:
