Twitter Feeds

Lorum Ipsum4
Lorum Ipsum5

Vision, Mission and Mandate

missionvision website

Facebook Feeds

Twitter Feeds

 

Afisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa ni Afisi huru iliyobuniwa kuzingatia Kipengee cha kifungu cha 260 cha Katiba ya Kenya, 2010 na kifungu cha 33 cha Sheria ya Vyama vya Kisiasa, 2011. Wajibu wake ni: kusajili, kudhibiti na kusimamia Hazina ya Vyama vya Kisiasa (PPF). Afisi hii, imesimamiwa na Msajili wa Vyama vya Kisiasa na manaibu wake watatu. Inao wafanyakazi weledi na wazoefu ambao humsaidia Msajili wa Vyama vya Kisiasa kutekeleza majukumu ya Afisi. Zaidi, katika kutekeleza majukumu yake, Afisi hushirikiana na wadau wengine wa serikali na wengine katika nyanja zisizo za kiserikali.

Sheria ya Vyama vya Kisiasa, 2011 (PPA, 2011) ikiambatanishwa  na Kanuni za Vyama vya Siasa (Usajili), 2019 inatoa ufafanuzi, mahitaji na masharti ya usajili wa vyama vya kisiasa. Usajili ni hatua mbili:

Masharti ya usajili wa muda:

Wanaonuia kusajili vyama  wanahitajika kutimiza yafuatayo:

 • Kutafuta jina: Jina, alama na rangi, kulingana na Kifungu 91 cha Katiba ya Kenya na kifungu cha 8 PPA 2011
 • Kuwasilisha katiba ya chama inayozingatia kifungu cha 9 cha PPA;
 • Kuwasilisha kumbukumbu za mkutano wa kwanza wa waanzilishi wa chama.
 • Ambatisho lililotiwa sahihi la ahadi ya kutii Kanuni za Maadili ya Vyama vya Kisiasa;
 • Wasilisha ombi kwa maandishi katika fomu iliyotengwa;
 • Kulipa ada iliyowekwa Shilingi elfu mia moja (100,000.00) inayolipwa kwa njia iliyotengwa ya kulipa.

Masharti ya usajili kamili:

 • Kupata wanachama wasiopungua elfu moja (1000) waliosajiliwa kama wapiga kura kutoka zaidi ya kaunti 24 za Kenya; Hawa wapaswa ambao wanapaswa kudhihirisha sura ya kimaeneo na makabila tofauti; usawa wa kijinsia na uwakilishi wa vikundi maalum ikiwa ni pamoja na wachache na waliotengwa;
 • Uundaji wa viongozi wa chama uthibitishe sura ya kimaeneo na makabila tofauti; usawa wa kijinsia na uwakilishi wa vikundi maalum ;
 • Viongozi wa chama wathibitishe kukidhi matakwa ya Sura ya 6 ya Katiba ya Kenya; na Sheria ya Uongozi na Uadilifu, 2012.

Wasilisha kwa Msajili katika muundo uliowekwa:

 • Orodha ya majina, anwani na maelezo ya wanachama wake wote;
 • Makao ya ofisi yake kuu iliyosajiliwa na matawi ya chama katika angalau kaunti 24 ;
 • Uainishaji wa data kwa misingi ya makundi maalum;
 • Ahadi ya kutii na Maadili ya Vyama vya Kisiasa;
 • Ada iliyowekwa Shilingi elfu mia tano (500,000.00) inayolipwa kwa njia iliyotengwa ya malipo.

Ada zinazolipwa kwa Afisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa ni:

 • Ada ya ukaguzi wa jina – Shilingi mia tano (500.00)
 • Usajili wa muda – Shilingi elfu mia moja (100,000.00)
 • Usajili kamili – Shilingi elfu mia tano (500,000.00)

Kufikia Februari, 2021, vyama vya kisiasa sabini na viwili (72) ndivyo vilikuwa vimesajiliwa kikamilifu. Vyama vilivyosajiliwa kwa muda hubadilika mara kwa mara kulingana na hatua vilivyopiga kutimiza mahitaji ya usajili kamili. Tizama wavuti wetu (www.orpp.or.ke).

Tuma malalamiko kwa njia ya barua pepe au barua ikiambatanishwa na nakala ya kitambulisho cha kitaifa / pasipoti halali kwa; This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. au kuileta katika makao makuu ya Afisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa iliyoko jumba la  Lion Place Waiyaki Way, ghorofa ya 1 au 4 au katika afisi za matawi zilizoorodheshwa kwenye wavuti wetu www.orpp.or.ke. Baada ya kutathminiwa, Msajili atafuta maelezo yako kutoka kwa rejista ya uanachama.

Wasilisha ilani iliyoandikwa ya kujiuzulu kwa njia ya barua pepe au barua ikiambatanishwa na nakala ya kitambulisho cha kitaifa au pasipoti halali kwa afisi ya chama husika kilichosajiliwa. Tuma nakala hiyo hiyo kwa Msajili wa Vyama vya Kisiasa kwa Ofisi ya Msajili au kupitia barua pepe; This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it..">This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.. Baada ya kutathminiwa, Msajili atafuta maelezo yako kutoka kwa rejista ya uanachama.

Hapana. Mtu anaweza tu kuwa mwanachama wa chama kimoja cha kisiasa. Mara tu jina la mtu limeingizwa kwenye rejista ya uanachama wa chama cha kisiasa, mtu huyo anakuwa mwanachama wa chama hicho hadi wakati ambapo jina hilo litaondolewa na kuingia kwenye rejista ya chama kingine cha kisiasa kulingana na mchakato wa kisheria.

 • Kujiuzulu kwa hiari - kwa kuwasilisha barua ya kujiuzulu kwa chama husika na / au Msajili.
 • Kutolewa - kupitia mbinu za chama zilizowekwa na chama husika;
 • “Kuonekana” - ambapo mwanachama anahusika kwa njia inayoonyesha kuwa yupo katika chama kingine cha kisiasa au anakiunga mkono, mbali na chama ambacho kiko katika mseto wa vyama.
 • Sababu za kiasilia - mtu anapofariki hukoma kuwa mwanachama wa chama cha kisiasa

IPPMS ni jukwaa la teknolojia mtandaoni uliobuniwa na Afisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa. Inachangia kusimamia na kudumisha rekodi za vyama vya kisiasa katika hifadhidata. Watumiaji walioidhinishwa kutoka vyama vya kisiasa wanao uwezo wa kutumia wenyewe jukwaa hili kupitia IPPMS katika kusimamia na kuwasilisha rekodi za uanachama kwa Msajili. Baadhi ya moduli zake ni kama: Ukaguzi wa uanachama na kujiuzulu chamani; upakiaji mwingi wa data ya uanachama; usimamizi wa mali ya vyama vya kisiasa na maafisa; rejista ya vyama vya kisiasa (orodha ya vya kisiasa vilivyosajiliwa na maelezo yao) na mengine mengi.

Chama cha kisiasa kinawajibika kudumisha rekodi sahihi katika ofisi yake kuu na ofisi za kaunti kwa muundo uliowekwa. Rekodi hizi ni pamoja na rejista ya wanachama wake; nakala ya katiba; sera na mipango ya usimamizi; vitabu vya hivi karibuni vya hesabu zilizokaguliwa; mali na rejista ya madeni kati ya rekodi zingine kama ilivyoainishwa katika sehemu ya 17, 18  ya PPA.

Rekodi zinapaswa kupatikana (pengine kwa ada iliyowekwa) kwa wanachama wake. Msajili anaweza kusababisha sababu za ukaguzi wa rekedi za vyama vya kisiasa kupitia utaratibu ulioainishwa chini ya kifungu 18 cha PPA

Mfumo wa kisheria na sera unafanyiwa kazi kufafanua mchakato na mamlaka kwa wagombea huru watakowekwa.

Mchakato hata hivyo, unahitaji mgombea kuwasilisha:

 • Barua ya maombi ya kuidhinishwa;
 • Nakala ya kitambulisho cha kitaifa au pasipoti halisi;
 • Ada ya shilingi mia tano (500).

Kwa ufanisi, mgombea anahimizwa kuwasilisha alama (kwa njia ya kielektroniki) anayotarajia kutumia kwa madhumuni ya uthibitishaji kabla kujiwasilisha katika IEBC.

Mara tu chama cha kisiasa kinapopata cheti cha usajili kamili kinapata hadhi ya kishirika inachokiwezesha kuendesha shughuli zake kisheria  kama shirika.

Chama kinawajibika:

 • Kuweka wagombea wake katika uchaguzi mkuu na chaguzi ndogo kilingana na muda uliwekwa na kanuni za Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC). Ikiwa chama kitashindwa kuweka mgombea yeyote kwenye uchaguzi kuu mara mbili mfululizo, kitafutiwa usajili wake.
 • Kuwasilisha mwitikio kwa maandishi kuhusu mali na madeni yake chini ya siku 60 kutoka tarehe ya usajili kamili.

Hapana. Chama cha kisiasa kilichosajiliwa kwa muda kimekatazwa kushiriki katika shughuli zozote za uchaguzi, pamoja na kuweka wagombea, kumpigia kampeni au kumpinga mgombea yeyote au kufanya mikutano yoyote ya hadhara.

Hata hivo, kina haki ya: kutangaza habari kukihusu kupitia njia zilizoidhinishwa na kutafuta ulinzi wa kiusalama na msaada kwa shughuli zake.

La. Katiba imeweka bayana kwamba mtu anaweza kugombea kama mgombea huru ikiwa yeye sio mwanachama wa chama chochote cha kisiasa miezi mitatu kabla ya siku ya uchaguzi.

Kwa ujumla, kuungana kunamaanisha vyama viwili au zaidi vya kisiasa vinapouunganisha shughuli zao na kuwa chama kimoja cha kisiasa. Sheria ya Vyama vya Kisiasa, 2011 inawezesha muungana wa vyama vya kisiasa ambapo vyama huvunjwa kwa minanjili ya kuunda chama kipya.

Sheria (PPA) inaeleza kwamba pale ambapo vyama vya kisiasa vinapokusudia kuungana, huweka kwa Msajili wa Vyama vya Kisiasa nyaraka zifuatazo:

 • makubaliano yaliyothibitishwa ya muungano
 • nyaraka zinazoonyesha kuwa sheria na taratibu za vyama vya kisiasa vinavyoungana zimefuatwa
 • Kumbukumbu za mkutano wa baraza simamizi la vyama vya kisiasa vinavyounganisha kuidhinisha kuungana.

Chama cha kisiasa basi kinapokea barua ya uthibitisho kutoka kwa Msajili na cheti cha usajili kamili kinatolewa.Vyama vilivyoungana basi hutolewa katika sajili zao, mali na madeni huhamishwa kwa chama kipya.

Mseto ni wakati ambapo vyama viwili au zaidi vinaungana kwa madhumuni ya kufuata lengo moja. Kuna aina mbili za miseto:

a) Miseto ya kabla ya uchaguzi

b) Miseto ya baada ya uchaguzi

Mseto unatofautiana na muungana kwani katika mseto, vyama hivyo vya kisiasa licha ya kuungana/ ushirikiano wao, huhifadhi vitambulisho huru vya kisheria unaodhihirika katika uongozi wao, katiba, wanachama kati ya vitambulisho vingine vya ushirika. Katika muungano, vyama husika huvunjwa kuunda chama kipya.

Chama cha kisiasa kinachokusudia kubadilisha au kurekebisha (katiba yake, kanuni, jina au anwani, eneo la ofisi kuu au ofisi ya kaunti, alama au kauli mbiu, anwani ya eneo lazima kiwasilishe kwa maandishi kwa mfumo uliowekwa kwa Msajili mabadiliko yaliyokusudiwa ndani ya muda uliowekwa (kifungu 20 cha PPA).

Vyama vya kisiasa lazima viwe vimeweka utaratibu wa ndani wa utatuzi wa migogoro katika miundo yao. Hii mara nyingi hupatikana katika katiba za vyama na / au sheria za uteuzi. Vyama vya kisiasa kwa hivyo, vinapaswa kuanzisha mchakato wa utatuzi wa mizozo kulingana na  utaratibu wa ndani wa kutatua mizozo uliowekwa. Wakati ambapo mzozo haujasuluhishwa kwa ndani, chama cha kisiasa au wanachama wanazo mbinu nyingenezo nje mwa chama za kutatua mizozo kama vile:

 • Jopo la Migogoro ya Vyama vya Kisiasa (PPDT);
 • Kamati ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uteuzi (IEBC);
 • Mahakama Kuu.

Mahakama ya Migogoro ya Vyama vya Kisiasa (PPDT) ni chombo cha kimahakama kilichoanzishwa chini ya Sheria ya Vyama vya Kisiasa. Jopo hili lina mamlaka ya kusikiliza:

 • Migogoro kati ya wanachama wa chama cha kisiasa;
 • Migogoro kati ya mwanachama wa chama cha kisiasa na chama cha kisiasa;
 • Migogoro kati ya vyama vya kisiasa;
 • Migogoro kati ya mgombea huru na chama cha kisiasa;
 • Migogoro kati ya washirika wa muungano;
 • Rufaa kutoka kwa maamuzi ya Msajili.

Sheria ya Vyama vya Kisiasa (PPA), 2011, Sehemu ya 38 inaanzisha Kamati ya Uhusiano ya Vyama vya Kisiasa (PPLC) katika ngazi ya kitaifa na kaunti. Kamati hii inashirikisha Afisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa, Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) na vyama vyote vya kisiasa vilivyosajiliwa kikamilifu. Jukumu lake ni kutoa jukwaa la majadiliano kati ya ORPP, IEBC na vyama vya kisiasa.

Vyama vya kisiasa vinapaswa kupata fedha zake kutoka kwa vyanzo halali. Vyanzo hivi ni pamoja na: ada ya uanachama, michango ya hiari, michango / wasia / misaada halali, mapato ya uwekezaji.

Vyama vya kisiasa vinavyofikia kiwango kilichotolewa chini ya kifungu cha 25 (2) ya PPA, 2011 vinastahiki ufadhili kutoka Hazina ya Vyama vya Kisiasa (PPF).

Chama cha kisiasa kitaweka wazi kwa Msajili maelezo kamili ya fedha zote au vyanzo vingine vya fedha zake.

Maafisa wa chama ndio wasimamizi wa vyama vya kisiasa. Vigezo vya kuchagua viongozi vimeainishwa katika katiba ya chama na / au kanuni kulingana na ratiba ya pili ya PPA, 2011.

Chama cha kisiasa kinapaswa kudumisha afisi za matawi zinazofanya kazi katika kaunti angalau 24 ambazo lazima ziashirie hadhi kama ile ya afisi kuu.