16 January, 2024: Notisi ya usajili wa muda

                                                                    

GoK logo

NOTISI YA USAJILI WA MUDA

Afisi ya Msajili wa Vyama vya Kisiasa (ORPP) imeanzishwa kupitia sehemu ya 33 ya Sheria ya Vyama Vya Kisasa, 2011 kama Afisi Huru kulingana na maana chini ya kipengee cha 260 cha Katiba ya Kenya, 2010.  Mamlaka ya ORPP ni kusajili, kudhibiti vyama vya Kisiasa na pia kusimamia Hazina ya Vyama vya Kisiasa.

Kulingana na sehemu ya 5(2) (a)ya Sheria ya Vyama Vya Kisiasa, 2011, Msajili wa Vyama vya Kisiasa yupo katika mchakato wa kuvisajili kwa muda vyama vifuatavyo. Maelezo yavyo ni kama yafuatavyo:

 

Jina Rangi za chama Ishara ya chama Kauli Mbiu                         Wanachama waanzilishi 
Imarisha Uchumi Party (IUP) Grey, dark teal blue, white and sunrise yellow Power line on post

IUP logo

“Inatuhusu”                1.    Alex Kanyi Kimani

2.    Maxwell Ochieng Nduko

3.    Patricia Nduleve Nzambu

Peoples Forum for Rebuilding Democracy (PFRD) Maroon, blue with red and green as minors Ballpoint pen with blue signature at the tip

pfrd

“The party to be, the change we want” 1.    Elizabeth Nthenya Joshua

2.    Benard Ochieng Adera

3.    Bilha Mukani Njoroge

Maelezo ya vyama vilivyopendekezwa yametolewa kwenye tovuti ya ORPP; www.orpp.or.ke

Pingamizi zozote zaweza kuwasilishwa kwa maandishi au kupelekwa kwa afisi za ORPP chini ya siku saba (7) kuanzia tarehe ya notisi hii, kupitia anwani:-

 

Msajili wa Vyama vya Kisiasa

Jumba la Lion Place, horofa  ya nne, barabara ya Waiyaki, Karuna close, Westlands

Sanduku la Posta, 1131-00606

Nairobi.

Barua pepe: registrar@orpp.or.ke

 

Ann N. Nderitu, CBS

Msajili wa Vyama vya Kisiasa

File Type: pdf
Categories: tenders
Downloads: 19
Scroll to Top